Friday, March 2, 2018

UHABA WA MAJI MOROGORO: Mama apambana na mamba, anusurika kuliwa, apoteza mwanae.

Siku sita kabla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, mwanamke mmoja amenusurika kuliwa na mamba wakati akiteka maji kwenye Mto Mgeta, Dakawa mkoani Morogoro, ikiwa ni madhara yanayotokana na kukosekana kwa huduma hiyo muhimu katika kijiji anachoishi.


Martha Malambi (25), baada ya shambulio hilo la Februari 17 lililosababisha kumpoteza mtoto wake wa kiume, Godfrey David (mwaka mmoja na miezi miwili) ambaye alikufa na baadaye maiti yake kusombwa na maji, kwa sasa anaendelea na matibabu katika Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Hospitali ya Muhimbili (MOI).


Ni saa 11:00 jioni katika kijiji cha Ukutu, Kata ya Bwakilachini, Martha akiwa amembeba mwanaye mgongoni, anafika katika Mto Mgeta baada ya kutembea mwendo wa nusu saa akitafuta maji.
“Nilikwenda mtoni kuchota majinikiwa nimembeba mwanangu, baada ya kujitwisha kichwani wakati naanza kutoka mtoni mamba mkubwa alinivamia kwa nyuma, alinikamata mguu sehemu ya msuli na paja akanivuta mtoni,” anasimulia Martha aliyepambana kijasiri na mambahuyo. 


Anasema baada ya kudondokamamba huyo alimvuta mpaka mtoni kwenye kina kirefu kisha kumzamisha chini ya maji, “Nilimhisi mwanangu namna alivyohangaika na maji aliyokuwa anakunywa baada ya sekunde chache alituibua tena juu hapohapo kitenge kikafunguka na mtoto akaondoka na maji, nilipata uchungu mkubwa,” anasema.


Anasema mamba alizidi kumbana zaidi na kumvutia bondeni. Wakati wa purukushani hizo alikuwa amembana mguu kwa meno yake na kuacha kiwiliwili, hivyo akawa anapiga kelele kuomba msaada huku akiendelea kupambana naye.


Mama huyo wa watoto wawili, huku mmoja aliyemuacha nyumbani akiwa na umri wa miaka mitano, anasema alitumia nguvu zaidi kupanua mdomo wa mamba ili kumpa maumivu, lakini aliendelea kumshinda nguvu kutokana na urefu wa mnyama huyo kuwa maradufu ya urefu wake.
“Kutokana na purukushani ile, aliona hajanidhibiti vizuri kwa sababu alinishika mguu mmoja, akajaribu kusogea kwenye kina kifupi cha maji ili anikamate vizuri,” anasimulia Martha.


Anasema hatua ya mamba huyo kusogea kwenye kina kifupi cha maji ya mto kutoka kina kirefu, kilimsaidia kuyafikia matete (magugu maji) hivyo aliyashika na kuyang’ang’ania kwa nguvu huku akiomba msaada kwa kupiga kelele.


Mwanamke huyo anasema ilikuwa bahati kwake, kwani kulikuwa na wavulana ambao hawakuwa mbali na mto huo ambao walisikia kelele za kuomba msaada na kuwahi eneo hilo, wawili wakiwa na magongo wawili wengine mapanga hivyo kuingia kwenye maji na kuanza kumshambulia mamba huyo.


Pamoja na msaada huo wa watu, mamba aliendelea kung’ang’ania mguu wake lakini mashambulizi yalivyozidi mamba alionekana kuchoka na kupata maumivu, hivyo kuuachia mguu na kuzama majini.
Hata hivyo, Martha anasema kabla hajaokolewa alikata tamaa kwani alihisi tayari amekufa: “Yule mamba mkubwa karibu mara mbili ya mwili wangu aliniogopesha sana, sikuwa nimewahi kumuona kwa macho yangu kabla ya siku hiyo. Viboko nawajua vizuri kwa sababu nimewahi kuwaona mara nyingi kijijini.


“Wale vijana walinichukua na kunipeleka nchi kavu baadaye Zahanati ya Lukumi, ambako walinipatia huduma usiku kucha, asubuhi ya Februari 18 walinisafisha vizuri maeneo yote yaliyoathiriwa na kucha na meno ya mamba huyo.”


Anasema kutokana na ukubwa wa majeraha hayo na mguu kuvunjika, alihamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambako baada ya kuhudumiwa takriban siku tano walimweleza kuwa tatizo lake inabidi apelekwe Muhimbili. Safari yake kwenda MOI ilianza akiwa yeye na wauguzi tu, alipofika alipokelewa na kupelekwa chumba cha upasuaji ambako alirekebishwa maeneo ya nyonga ambayo pia yaliathiriwa.


“Nimefika MOI nikiwa peke yangu. Sina ndugu hapa Dar es Salaam wala ndugu yeyote kutoka nyumbani ambaye amefika hospitali tangu siku hiyo. Nashukuru wauguzi na madaktari wamekuwa wakinisaidia wakati wote, ninapata matibabu vizuri, ninapata chakula, nashukuru kwa hilo” anasema na kusisitiza kuwa familia yake ni maskini, hivyo hana mawasiliano nao kwani simu aliyoitegemea ilisombwa na maji.


Uhaba wa maji Ukutu

Martha anayeishi na wazazi wake kijijini hapo, anasema hawawezi kuepuka kufuata maji mtoni kwa kuwa hakuna chanzo kingine cha maji kijijini zaidi ya mto Mgeta, miaka yote wamekuwa wakichota maji hapo.


“Miaka yote tuliyoishi pale hatujawahi kusikia tukio la shambulio la mamba eneo hilo. Nimezaliwa na kukulia hapo na wazazi wangu pia wamezaliwa na kukulia hapohapo. Wanyama wapo kwenye huo mto, hasa viboko, maji yakijaa wanatembea hadi kwenye makazi ya watu lakini mamba hawakuwahi kuwapo eneo hilo zaidi na maeneo ya mbali,” anasema.


Martha ambaye ni mkulima wa mpunga na mahindi anaainisha kuwa miaka kadhaa iliyopita, kulikuwa na mabomba matatu ya jumuiya katika kijiji chao lakini kwa zaidi ya miaka minne sasa hayafanyi kazi tangu yalipoharibika.


MOI kumfanyia upasuaji

Daktari bingwa mwandamizi wa upasuaji mifupa MOI, Paul Marealle anathibitisha kumpokea Martha na kwamba, tayari wameanza kumpatia matibabu kinachosubiriwa ni upasuaji.
“Alipata jeraha kubwa la kuvunjika mfupa wa paja na vidonda kwenye eneo la paja na mguu wa kulia,” anasema Dk Marealle na kuongeza:


“Wagonjwa wengi wa namna hii wanakuwa wamepoteza damu, hivyo tunawaongezea na tunawapatia huduma ya karibu kabisa, kwa sasa tumemtibu na majeraha yake yamepona, kwa hivyo tutamrudisha chumba cha upasuaji kushughulika na mfupa wake ambao umevujika.
“Tunajaribu kuondoa uchafu na sumu yote ambayo inaonekana kwa macho na wanawekwa kwenye antibiotic maalumu na kurudishwa chumba cha upasuaji mara kwa mara.”


Huduma kwa majeruhi wa mamba
Anasema huduma ya kwanza ambayo mgonjwa aliyeng’atwa na mamba anafaa kupewa ni kuzuia damu isitoke, kwa kuwa hupoteza damu nyingi huku akisisitiza majeruhi yeyote lazima aangaliwe kwa namna anavyobebwa na kuhudumiwa kulingana na majeraha yake.


“Mamba anakula vitu vingi hivyo ana sumu kali ya vijidudu vinavyokaa kwenye meno yake vinavyotokana na uchafu, kwa hivyo kitu cha kwanza lazima kuhakikisha kidonda kimesafishwa vizuri hata na maji yanayotiririka,” alisema.


Dk Marealle anasema iwapo mgonjwa asipopewa tiba ya antibiotic kwa haraka, kinachoweza kutokea ni kufa kwa ngozi, misuli na mishipa ya fahamu hivyo madhara yake nikukatwa sehemu husika.


Cc: Jf

Wednesday, February 28, 2018

UTARATIBU WA MKATOLIKI AINGIAPO HADI ATOKAPO KANISANI


  •  Ninapoingia kanisani nachovya maji ya baraka na kusema

"Unitakase Ee Bwana mimi na uovu wangu wote, ili nipate kustahili kushiriki ibada takatifu' Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu" Amina! 




  • Ninapiga goti huku nikisema"Mungu wangu na Bwana wangu"

  • Nikiinuka nasema

"Nitakusifu na kukuabudu katika Ekaristi takatifu"

  • Naenda mpaka kwenye bench, napiga magoti au nakaa nikiwa mimeinamisha kichwa (kama mabenchi yameisha nabaki nimejisimamia) huku nikitoa nia yangu ya kusali misa siku hiyo, mfano

"Ee Mungu, ninaungana nawe na jeshi lote la mbinguni, pamoja na Mama Bikira Maria, nikiwa na nia ya kumwombea mama yangu ambaye ni mgonjwa, jirani yangu ambaye mpaka sasa hatuelewani na pia familia yetu ambayo haina amani, Mungu kupitia misa hii rejesha hali ya mama yangu, rejesha uelewano na jirani yangu, na pia rejesha amani ya familia yetu pamoja na familia zote ambazo hazina amani"

  • Ninaendelea na misa na Kushiriki litrujia kikamilifu

  • Mwisho wakati wa kuondoka nachovya maji ya baraka nikisema

"Unilinde Ee Mwenyezi Mungu, nikapate kuwa mfano katika jamii yangu, na nikushuhudie katika matendo yangu"
(Hapo nachovya maji ya baraka na kufanya ishara ya msalaba) "Kwa jina la Baba na la Mwana na la RohoMtakatifu, amina"


TRENI YAPATA AJALI UVINZA. HAKUNA VIFO NI MAJERUHI WATATU

TRENI ya abiria iliyokuwa ikisafiri kutoka Tabora kwenda Kigoma imeanguka mchana huu kati ya stesheni ya Malagarasi na Uvinza katika eneo la Kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Ferdinand Mtui amethibitisha.

Hadi sasa hakuna kifo kilichothibitishwa wala idadi ya majeruhi, kamanda huyo ameahidi kutoa taarifa zaidi baadaye baada ya kufika eneo la tukio.

Ajali hiyo imetokea mchana huu Februari 28, 2018, baada ya mabehewa mawili ya mbele na kichwa chake kuacha njia na kuanguka.
========

Watu watatu wamejeruhiwa

Ajali hiyo imesababishwa na kichwa cha treni kuacha njia na mabehewa mawili kuanguka, shirika la habari la kibinafsi la Azam limeripoti.

Kaimu meneja wa wamawasiliano wa Shirika la Reli la Tanzania (TRL) Mohamed Mapondela ameambia BBC kwamba watu watatu wamejeruhiwa.

"Sababu ya ajali bado haijafahamika lakini, timu ya kutathmini ajali iko njiani kuelekea eneo la tukio," amesema.

Ajali ilitokea majira ya saa saba na dakika hamsini mchana eneo la katikati ya stesheni ya Malagarasi na Uvinza.

"Tathmini kamili ya ajali itatolewa pale ambapo mabehewa yatakuwa yameinuliwa."

Bw Mapondela amesema eneo hilo si kwamba ni baya na halina historia ya kupata ajali yoyote ile, ndio maana ni vigumu kusema nini hasa kinaweza kuwa chanzo cha ajali.

Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe ameandika kwenye Facebook kwamba amezungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma na kufahamishwa kwamba chanzo cha ajali ni injini kupoteza njia kufuatia mchanga uliokuwa kwenye njia ya reli. "Naomba uchunguzi ufanyike ili kuona kama mchanga ule ni sababu ya mvua kubwa zinazonyesha ama la. Treni ndio usafiri wa wanyonge wengi mkoani kwetu hivyo ajali za namna hii zinastusha na kuogopesha. Natoa pole sana kwa wana Kigoma na Watanzania wengine," amesema.

Cc: jf

PAMBANIENI UHURU: anaandika baba askofu Steven Munga

Uhuru si zawadi tunayopewa na watawala bali ni haki ya asili ya kilamtu kwa sababu tuliumbwa nayo. NI HAKI YA ASILI!!! 

Kiuhalisia tawala za kidunia maranyingi hulenga katika kupora uhuruhuo ili wawatawale watu kamawapendavyo. Lakini hivyo si sawa. Hata Mungu alipowaumba Adamu na Hawa aliwapa uhuru wa kutosha wa kufanya maamuzi na uchaguzi (Mwanzo mlango wa 1 na wa 2). 

Ni ubaya na uovu pale tu uhuru huo unapotumika vibaya kwa lengo la kuingilia, kukandamiza na kuhatarisha uhuru na maisha ya wengine. Hii ndio sababu zipo katiba na sheria za nchi huru pamoja na maazimio ya kimataifa vinavyotungwa ili kulinda uhuru huo. 

Uhuru wetu ni haki na kipawa chaasili tulichopewa na muumba wetu
Ni wajibu wako kupambana na yeyote anayejaribu kukunyang'anya uhuruwako ambao ni haki yako ya asili.

Tuesday, February 27, 2018

Aida olomi wenzake kufikishwa mahakamani Leo baada ya mahakama Mkuu kungilia

Anaandika waliki  Alex massaba

Nipenda kuwapa taarifa juu ya watu wetu watatu (Aida Olomi, Isaack lomanus, na Erick John) wanaoshikiliwa na jeshi la polisi katika kituo cha polisi cha osterbay, jijini Dar es salaam kwa takribani siku 11 sasa, na kwa muda wote huo polisi imewanyima dhamana.

Timu ya Mawakili tuliamua kufungua kesi Mahakama Kuu kuwashitaki IGP na Mwanasheria Mkuu (AG) kwa kosa la kuendelea kuwashikilia wateja wetu kinyume na Sheria za nchi. Mbaya kuliko lote hawana kibali chochote kutoka kwa hakimu cha kuendelea kukaa nao kituoni.

Tumshukuru mwenyezi Mungu kuwa hatua hii ya Mahakama Kuu tumefanikiwa kupata summons na tumemsave IGP na AG, ambapo kesi imepangwa kusikilizwa kesho SAA saba mchana Mbele ya Jaji Arufani. 

Aidha, kuna taarifa kuwa polisi wanajiandaa kuwapeleka Mahakamani Kisutu mida ya asubuhi kwa siri ili kukwepa waandishi Wa Habari.

Niwaombe makamanda wote kesho kuazia asubuhi tujitokeze kwa wingi na niombe tugawanyike wengine tuanzie osterbay Polisi na wengine tutangulie Mahakamani Kisutu.

Swala la wadhamini naomba lipewe kipaumbele ni aibu kubwa sana tunapofanyakazi kubwa na ngumu ya kuwezesha watu wetu kufikishwa Mahakamani halafu wanakosa wadhamini. Naomba madiwani wetu wajitokeze kwa wingi.

Aidha, kuna taarifa kuwa serikali wanajipanga kuja na kiapo cha kuzuia dhamana ya watu wetu, sisi Mawakili tumejipanga kupambana na hilo.

Zaidi ya yote nawashukuru watu wote kwa namna ambapo kila mmoja wetu amepambana kuhakikisha kwamba wenzetu hawa wanakuwa huru na Mungu akipenda muda mfupi ujao tutakuwa na uraiani.

Wakili Alex Massaba
27/02/2018








My take: za kuambiwa changanya na za kwako


Waziri Wa Tamisemi aagiza ujenzi Wa viwanda 100 kila mkoa.




WAZIRI SELEMANI JAFO ATAKA VIWANDA VIPYA 2600 KATIKA MIKOA 26 IFIKAPO DESEMBA 2018
--------------------------------------------------
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Seleman Jafo amewataka Wakuu wa Mikoa nchini kuhakikisha kuwa kila mmoja anajenga viwanda vipya 100 kuanzia Desemba 2017 hadi Desemba 2018.

Akizungumza na Wakuu wa mikoa wapya walioapishwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam, na kufanya nao mazungumzo katika Ofisi ya TAMISEMI Jijini Dar es Salaam, Waziri Jafo alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa ifikapo Desemba 2018, mikoa yote 26 ya Tanzania Bara inakuwa na viwanda vipya 2600.

Waziri Jafo alisema Serikali ya Awamu ya Tano imekusudia kufikia nchi ya uchumi wa kipato cha kati kupitia ujenzi wa viwanda, hivyo aliwataka wakuu wa Mikoa yote nchini kuhakikisha kuwa wanaibua viwanda vidogo na vya kati kwa kuhamasisha ushiriki wa Viongozi ndani ya mikoa na wananchi wote katika maeneo yao ya utawala.

Aliongeza kuwa katika kusimamia utekelezaji wa agizo hilo, Ofisi yake itaweka utaratibu maalum wa kupima utendaji kazi wa Kila Kiongozi wa Mkoa katika kuangalia ushiriki wake wakuwajengea hamasa Viongozi wa chini wakiwemo Wakuu wa W ilaya na wananchi.

“Serikali itatoa vyeti kwa Mikoa yote itakayofanya vizuri katika ujenzi wa viwanda, hatua hii inalenga kutoa motisha kwa mikoa iliyobaki kuweza kujifunza na kubaini mbinu mbadala katika kuibua viwanda ili kuweza kuwakomboa kiuchumi wananchi” alisema Jafo.

Kwa mujibu wa Waziri Jafo alisema katika kufanikisha dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini Serikali inaendelea kuweka mkazo na kipaumbele katika upatikanaji wa malighafi za kilimo, na hivyo kuwataka Wakuu wa Mikoa kuhakikisha kuwa Maafisa Ugani wanatekeleza vyema majukumu yao ya kazi.

Aidha Jafo aliwataka Wakuu wa Mikoa nchini kusimamia vyema makusanyo ya fedha za ndani zinazokusanywa katika Halmashauri zote nchini na kutumia vyema fedha za asilimia 5 zilizotengwa katika halmashauri kuwawezesha na kuhamasisha wananchi kupata mikopo ili kuwawezesha kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Waziri Jafo pia aliwataka Wakuu wa Mikoa kuwaelekeza Maafisa Maendeleo ya Jamii nchini kuweza kuhamasisha wananchi kujiunga katika vikundi vya ushirika ili weweze kupatiwa mikopo kupitia mifuko ya fedha inayotolewa na Serikali na hivyo kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima alisema ili kufanikisha dhana ya uchumi wa viwanda, Serikali haina budi kuwapa msukumo na ushirikiano wa karibu Wanasayansi ili kuwawezesha kuibua viwanda vingi zaidi pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa malighafi za kilimo nchini.

Friday, June 9, 2017

Mdudu hatari aonekena kwenye mboga

Mdudu hata anayepatikana Kwenye mboga za majani anayejulikana kama mdudumtu ameonekana maeneo yamwatulole Geita. Wakazi wa mtaahuo wanasema huwa. Anakaa. Kwenye

UHABA WA MAJI MOROGORO: Mama apambana na mamba, anusurika kuliwa, apoteza mwanae.

Siku sita kabla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake  Duniani, mwanamke mmoja amenusurika kuliwa na mamba wakati akiteka maji kwenye Mto Mget...