Wednesday, February 28, 2018

TRENI YAPATA AJALI UVINZA. HAKUNA VIFO NI MAJERUHI WATATU

TRENI ya abiria iliyokuwa ikisafiri kutoka Tabora kwenda Kigoma imeanguka mchana huu kati ya stesheni ya Malagarasi na Uvinza katika eneo la Kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Ferdinand Mtui amethibitisha.

Hadi sasa hakuna kifo kilichothibitishwa wala idadi ya majeruhi, kamanda huyo ameahidi kutoa taarifa zaidi baadaye baada ya kufika eneo la tukio.

Ajali hiyo imetokea mchana huu Februari 28, 2018, baada ya mabehewa mawili ya mbele na kichwa chake kuacha njia na kuanguka.
========

Watu watatu wamejeruhiwa

Ajali hiyo imesababishwa na kichwa cha treni kuacha njia na mabehewa mawili kuanguka, shirika la habari la kibinafsi la Azam limeripoti.

Kaimu meneja wa wamawasiliano wa Shirika la Reli la Tanzania (TRL) Mohamed Mapondela ameambia BBC kwamba watu watatu wamejeruhiwa.

"Sababu ya ajali bado haijafahamika lakini, timu ya kutathmini ajali iko njiani kuelekea eneo la tukio," amesema.

Ajali ilitokea majira ya saa saba na dakika hamsini mchana eneo la katikati ya stesheni ya Malagarasi na Uvinza.

"Tathmini kamili ya ajali itatolewa pale ambapo mabehewa yatakuwa yameinuliwa."

Bw Mapondela amesema eneo hilo si kwamba ni baya na halina historia ya kupata ajali yoyote ile, ndio maana ni vigumu kusema nini hasa kinaweza kuwa chanzo cha ajali.

Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe ameandika kwenye Facebook kwamba amezungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma na kufahamishwa kwamba chanzo cha ajali ni injini kupoteza njia kufuatia mchanga uliokuwa kwenye njia ya reli. "Naomba uchunguzi ufanyike ili kuona kama mchanga ule ni sababu ya mvua kubwa zinazonyesha ama la. Treni ndio usafiri wa wanyonge wengi mkoani kwetu hivyo ajali za namna hii zinastusha na kuogopesha. Natoa pole sana kwa wana Kigoma na Watanzania wengine," amesema.

Cc: jf

No comments:

Post a Comment

UHABA WA MAJI MOROGORO: Mama apambana na mamba, anusurika kuliwa, apoteza mwanae.

Siku sita kabla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake  Duniani, mwanamke mmoja amenusurika kuliwa na mamba wakati akiteka maji kwenye Mto Mget...